Story by Ali Chete-
Michuano ya Shahbal Super Cup imeingia hatua ya 16 bora baada ya timu 128 kushiriki katika ligi hiyo inayoendelea katika kaunti ya Mombasa.
Akizungumza na Wanahabari Mwenyekiti wa michuano hiyo Alami Ahmed Abdallah amesema timu hizo zimeonyesha ushirikiano wa hali ya juu na bado wana matumaini kwamba ushirikiano huo utaendelea ili kukuza talanta za vijana.
Abdallah amedokeza kwamba licha ya kuwepo na chanagamoto mbalimbali ikiwemo ukosefu wa nidhamu kwa baadhi ya wachezaji, ligi hiyo bado inaendelea.
Kwa upande wake Katibu mkuu wa michuano hiyo Gilbert Wesonga amesema kila gatuzi dogo katika kaunti hiyo lina timu ambazo zinawakilisha gatuzi hizo.
Hata hivyo michuano hiyo ya 16 bora imeratibiwa kuanza rasmi tarehe 5 mwezi Machi huku mchuano wa kwanza ukiwa Somali Youth kutoka Mvita wakikipiga dhidi ya Hope Rangers katika uga wa Serani huku finali ya mchuano huo ukiratibiwa kuzaragazwa tarehe 20 mwezi huu wa Machi.