Story by Mwahoka Mtsumi –
Mhubiri wa Muungano wa Makanisa ya Synagogue Church of All Nation, Temitope Balogun Joshua, kwa jina maarufu T.B Joshua ameaga dunia.
Uongozi wa Muungano wa makanisa hayo umethibitisha kutokea kwa kifo chake.
Katika taarifa iliotolewa na uongozi wa Muungana wa Makanisa hayo, imesema Kiongozi huyo wa kidini amefariki dunia siku ya Jumamosi tarehe 15 mwezi huu, japo Muungano huo wa umekosa kuweka wazi kiini cha kifo chake.
Mhubiri huyo wa taifa la Nigeria ambaye pia ni muanzilishi wa runinga ya kidini ya Emmanuel Tv ametambulika sana na wengi kutokana na unabii na mahubiri yake ya kuziunganisha jamii mbalimbali katika bara la afrika kupitia neno la Mungu.
Mwendazake TB Joshua ameaga dunia akiwa na umri wa miaka 57.