Picha kwa hisani –
Mgomo wa wahudumu wa afya katika hospitali za umma kote nchini umeingia siku yake ya pili hii leo.
Katika kaunti ya Mombasa tayari walikuwa wanaendelea na mgomo wao katika kaunti hiyo ambao umeingia juma la nne sasa, wakilalamikia nyongeza ya mishahara na hii leo wamejiunga na wenzao kwa mgomo wa kitaifa ambao umeingia siku yake ya pili.
Wakiongozwa na Katibu wa muungao wa madaktari katika kaunti hiyo Peter Maroko, wahudumu hao wamesema wataendelea na mgomo hadi pale matakwa yao yatakapo shuhulikiwa.
Kwa upande wake mwakilishi wa kike kaunti ya Murang’a Sabina Chege ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya afya katika bunge la kitaifa, akiwarai washikadau kuja pamoja kujadili swala hili ili kupata suluhu.