Mgogoro wa ardhi umezuka upya huko Maweni katika eneo bunge la Kilifi kusini, huku wakaazi wanaoishi katika ardhi hio wakitaka suluhu ya haraka kuhusu mzozo huo.
Wakiongozwa na Mwenyekiti wao Tsongo Mwarua Kajimbi wakaazi hao wamedai kwamba ndio wamiliki halisi wa ardhi hiyo yenye hekari 161 na sio bwenyenye mmoja anayedai anamiliki ardhi hiyo.
Kajimbi amehoji kwamba mgogoro huo umekuwa mahakamani na Wakaazi wakaishinda kesi hiyo,akisema kuna njama ya kuwafurusha kwenye makaazi hayo kwani bwenyenye huyo tayari ameanza kuzibomoa nyumba zao.
Mmoja wa wakaazi hao Megi Kombo amesema shamba hilo kwa sasa liko chini ya umiliki wa Serikali, akitaka Serikali kumkabili mwekezaji huyo anayelenga kuwatimua kwenye ardhi yao asilia.
Utata huo wa ardhi umedumu kwa miaka 20 sasa.