Picha kwa Hisani –
Seneta wa Taita taveta Jones Mwaruma ameutaja ukosefu wa ushirikiano miongoni mwa viongozi wa ukanda wa pwani kama chanzo cha kutosuluhishwa kwa matatizo yanayowakumba wapwani.
Akizungumza na wanahabari Mwaruma amesema mgawanyiko huo wa viongozi pia umesambaratisha vyama vya kisiasa vya pwani hali inayochangia eneo hili kusalia nyuma kimaendeleo.
Mwaruma amesema licha ya kwamba kwa sasa viongozi wa pwani wanaendeleza mchakato wa kuunda chama cha kisiasa cha pwani,lazima wakaazi wa ukanda huu wahusishwe kikamilifu.