Story by Gabriel Mwaganjoni –
Mfumo wa elimu wa 2-6-6-3 umetajwa kama afueni kwa watoto hasa kuhusu masomo ya mazingira shuleni.
Mwanamazingira na anayesimamia mradi wa mazingira katika shule za Agha Khan kaunti ya Mombasa Joe Karanja amesema mfumo huo umeyaangazia vyema maswala ya mazingira na unapaswa kukumbatiwa katika kulinusuru taifa hili dhidi ya mabadiliko ya anga.
Akizungumza katika kaunti ya Mombasa, Karanja ameitaka Wizara ya Elimu kuhakikisha maswala ya mazingira yanaangaziwa na kizazi kichanga kunahimizwa kukumbatia umuhimu wa uhifadhi wa mazingira.
Karanja hata hivyo amehoji kwamba huenda mfumo huo ukose kuzaa matunda endapo wanafunzi hawatashirikishwa katika elimu zoezi kwa kujumuishwa katika miradi mbalimbali ya kimazingira mashinani.