Story by Gabriel Mwaganjoni-
Mfanyabiashara mmoja amefikishwa katika Mahakama ya Taveta, kaunti ya Taita Taveta akikabiliwa na mashtaka ya kuingiza Mahindi humu nchini na kukwepa kulipa ushuru.
Mahakama imefahamishwa kwamba mnamo kati ya mwaka wa 2014 na 2019 mshukiwa kwa jina Wilson Kiplagat Chesang aliingiza Mahindi humu nchini yenye thamani ya shilingi milioni 500.9 kutoka nchini Tanzania na hakuyalipia ushuru.
Akiwa mbele ya Hakimu Louser Chebeni, Chesang amekana mashtaka hayo na akaachiliwa kwa dhamana ya shilingi milioni moja na mdhamini wa kiasi sawa na hicho au pesa taslimu shilingi nusu milioni.
Kesi hiyo imeratibiwa kusikizwa Februari, 28 mwaka huu.