Story by Gabriel Mwaganjoni-
Mfanyabiashara mmoja amefikishwa katika Mahakama ya Mombasa akikabiliwa na kosa la kuingiza bidhaa kisiri humu nchini kupitia maji makuu ya bahari hindi.
Inadaiwa kwamba Yusuf Mohammed Abdalla alifanya kosa hilo mnamo mwezi Mei tarehe 17 mwaka huu akiwa ametoa mitungi 77 ya mafuta ya uto sawa na tani 17 za vyuma vikuu kuu kutoka Jumba Land, Somalia.
Mohammed alinaswa na Maafisa wa usalama sawia na wale wa mamlaka ya ushuru nchini KRA akijaribu kupakua bidhaa hizo kisiri ili zifike katika bandari ya Mombasa akiwa na lengo la kukwepa kulipa ushuru.
Hata hivyo, mshukiwa amekanusha shtaka hilo la kuingiza bidhaa za thamani ya takribani shilingi milioni moja kinyume cha sheria.
Mahakama imemwachilia mshukiwa huyo kwa dhamana ya shilingi nusu milioni na mdhamini wa kiasi sawa na hicho.
Kesi hiyo itatajwa tena Oktoba, 17 mwaka huu.