Story by Gabriel Mwaganjoni –
Mfanyabiashara mmoja amefikishwa katika Mahakama ya Mombasa akikabiliwa na kosa na kukwepa kulipa ushuru.
Mahakama imearifiwa kwamba Mfanyabiashara huyo Robert Muthumbi Muriuki ambaye ni Mkurugenzi wa kampuni ya Landmark Concepts aliingiza trekta maalum la kuchimba ndani ya maji na kukwepa kulipa ushuru wa kima cha shilingi milioni 12.4
Mahakama pia imefahamishwa kwamba mfanyabiashara huyo alitenda uhalifu huo kati ya tarehe 12 ya mwezi Oktoba mwaka wa 2018 na tarehe 2 mwezi Novemba mwaka wa 2019.
Akiwa mbele ya Hakimu Rita Amwayi, mshukiwa amekanusha mashtaka hayo na kuachiliwa kwa dhamana ya shilingi milioni moja au pesa taslimu shilingi laki mbili.
Kesi hiyo itaanza kusikizwa mnamo Disemba tarehe 6 mwaka huu.