Picha kwa hisani –
Harmonize amesimulia jinsi meneja wake Jembe ni Jembe alivyo msaidia kulipa pesa alizolipishwa na usimamizi wake wa zamani WCB chini ya mwanamuziki nyota wa Bongo Fleva Diamond Platnumz.
Harmonize amewasisimua mashabiki wake kwenye mitandao baada ya kuelezea kwamba wakati anaambiwa alipe pesa hizo, hakuwa nazo ila Jembe alimpa kiasi cha shilingi milioni 100 za Tanzania na yeye akaongezea milioni 200 kwa kuuza baadhi ya vitu vyake alivyokuwa ameviwekeza nchini Italia kwa mke wake.
Mbali na hilo Harmonzie ameongeza kuwa kuna watu wengi sana wana waza kuwa Jembe yupo kwake kwa ajili ya pesa, amekanusha na kusema hilo sio bali Jembe ndio mtu alimfanya asimame mpaka hapa alipo.
Pia ameongeza kuwa yeye anampenda sana Diamond akimaanisha uongozi wake wa zamani na kusema upendo alionao juu ya uongozi huo Mungu pekee ndiye anajua.