Picha kwa hisani –
Wataalum wa maswala ya Katiba na wasomi kutoka ukanda wa Pwani walikongamana katika ukumbi wa Star of the Sea kule Mombasa hapo jana na kuyachambua kwa kina maswala yaliyomo ndani ya ripoti ya BBI.
Wakiongozwa na Msomi Profesa Halim Shauri, na Maurice Mwaru, wamefichua maswala tata yanayowakumba wapwani ambayo kulingana na wasomi hao maswala hayo yamekosa kujumuishwa ndani ya ripoti hiyo licha ya kupendekezwa na viongozi wa Pwani.