Picha kwa Hisani –
Baraza la vyombo vya habari nchini MCK limewataka wanahabari kuzingatia usalama wao wanapokua nyanjani wakati huu ambapo joto la kisiasa limepamba moto nchini.
Afisa mkuu mtendaji wa baraza hilo David Omwoyo amesema wanahabari wako katika hatari kupata madhara ya kiafya wanapofatilia taarifa za ghasia hasa kunapotokea ufyatulianaji risasi sawa na kurushwa vitoa machozi.
Omwoyo amesema kuna haja ya wamiliki wa vyombo vya habari nchini kuwapa vifaa vya kujikinga wanahabari wa nyanjani ili kuwaepusha na madhara yanayohatarisha maisha yao.
Baraza hilo la wanahabari limeyataja maeneo ya Garissa na Tanariver kama yalioyo hatari zaidi na kwamba wanahabari wa maeneo hayo wanafaa kuchukua tahadhari.