Story by Janet Shume –
Baraza la vyombo vya habari nchini MCK limetangaza kuzinduliwa kwa mradi wa mafunzo ya muda kwa wanafunzi wanaosomea taalum ya uanahabari katika vyuo vikuu na taasisi tajika za kielimu humu nchini.
Afisa mkuu mtendaji wa baraza hilo David Omwoyo amesema mpango huo unalenga kuhakikisha wanafunzi 400 wananufaika kwa kupata nafasi za mafunzo ya muda katika vyomba vya habari nchini.
Omwoyo ametaja hatua hiyo kama inayolenga kuimarisha uhusiano kati ya sekta ya uanahabari na taasisi mbalimbali za mafunzo katika kuhakikisha wanafunzi hao wanapata mafunzo mwafaka kulingana na kanuni za baraza hilo.
Hata hivyo amewataka wakurungezi wa vituo mbalimbali vya habari kushirikiana na baraza hilo katika mradi huo, akisema baraza la MCK litahakikisha linatoa shilingi elfu 15 kwa ajili ya matumizi ya kila mwezi ya wanafunzi hao.