Story by Jumaa Mwakunyinyia –
Baraza la vyombo vya habari nchini MCK limefanya vikao vya kukusanya maoni ya Wanahabari na wadau wengine husika kuhusu sheria na maadili ya uanahabari.
Naibu mkurugenzi wa idara ya mafunzo ya Wanahabari katika baraza hilo Christine Nguku amesema wanalenga kufanyia marekebisho sheria za uanahabari ili kuangazia sekta mbali mbali za uandishi ikiwemo ile ya mtandao.
Christine amesema wataandaa ripoti kamili yenye muongozo wa uandishi baada ya kukusanya maoni hayo na kuiwasilisha bungeni kujadiliwa kabla ya kuidhinishwa na kuwa sheria.
Zoezi hilo ambalo liling’oa nanga linaendelezwa katika kaunti mbalimbali nchini ikiwemo kaunti za Pwani.