Picha kwa Hisani
Wawakilishi wa wadi katika kaunti ya Nairobi, sasa wanatishia kumtimua mamlakani Gavana wa kaunti hiyo Mike Mbuvi Sonko kutokana na kushindwa kuwajibikia majukumu yake.
Wakiongozwa na Mwakilishi wa wadi ya Embakasi katika kaunti ya Nairobi Ogado Okumu, viongozi hao wamempaka Gavana Sonko makataa ya siku 14 kumteua Naibu Gavana wa kaunti hiyo la sivyo watamtimua uongozini.
Okumu amesema tabia ya Gavana Sonko kukosoa uongozi wa Nairobi Metropolitan chini ya Meja generali Mohamed Badi, ni kutafuta mbinu ya kuvuruga maendeleo ya kaunti ya Nairobi.
Wawakilishi hao wa wadi wamemtaka Rais Uhuru Kenyatta, Chama cha Jubilee na viongozi husika kuingilia kati swala hilo na kumteua Naibu Gavana wa Nairobi la sivyo watanzisha mchakato wa kumtia Gavana Sonko Mamlakani.