Story by Taalia Kwekwe-
Shirika la kijamii la Organization For Creative Leadership kaunti ya Kwale ni mojawapo ya mashirika ambayo yametumia njia ya upatanishi kama njia mbadala ya kutatua mizozo katika jamii.
Mmoja wa Waanzilishi wa shirika hilo Rashid Mbwiza amesema upatanishi umesaidia pakubwa kudumisha siri wakati wa kutatua mizozo na vile vile kudumisha uhusiano mwema katika jamii.
Mbizwa ambaye pia ni Wakili, amesema wananchi wanafaa pia kutumia njia za upatanishi katika kutatua mizozo na wala sio kukimbilia Mahakamani pindi kunapotokea mizozo.
Mbwiza amesema kesi ambazo zinaweza kutatuliwa kupitia njia za upatanishi ni kesi kama zile za kifamilia hasa haki za watoto na mahitaji yao, kesi za mashamba pamoja na zinazohusu waajiri na waajiriwa.