Mbunge wa Rabai William amejitokeza wazi wazi na kudai kwamba iwapo marekebisho ya katiba hayataachiwa wananchi kutoa maoni yao basi katu hatayaunga mkono marekebisho husika.
Mbunge huyo amefutilia mbali mapendekezo ya kinara wa Third Party Alliance, Ekuro Okoth na kuitaja kama ya kibinafsi hivyo basi kuapa kutoiunga mkono iwapo hatashirikisha wananchi mashinani.
Kamoti mesema hatua ya kutaka nafasi fulani za uongozi kuondolewa haiungi mkono kwa vyovyote vile na kusema kwamba wananchi lazima wawakilishwe kikamilifu.