Picha kwa Hisani –
Mbunge wa Mvita Abdulswamad Shariff Nassir ametangaza bayana kwamba sasa atauwania ugavana wa Kaunti ya Mombasa katika uchaguzi mkuu wa mwaka wa 2022.
Nassir amesema atapambana na yeyote yule atakayeingia kwenye kinyang’anyiro hicho cha Ugavana wa Kaunti ya Mombasa.
Wakati uo huo, Nassir ameapa kumuunga mkono kikamilifu gavana Mombasa Ali Hassan Joho katika azma yake ya kuunyakua urais wa nchi kwenye uchaguzi mkuu ujao.
Kwa upande wake gavana Joho amethibitisha kwa mara nyengine tena kwamba atawania urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka wa 2022.