Story by Gabriel Mwaganjoni –
Mbunge wa Mvita Abdulswamad Sharif Nassir amewahimiza wakaazi wa kaunti ya Mombasa kujitenga na wanasiasa wachochezi na wasio na nia yoyote ya kuimarisha malengo yao.
Nassir amesema mara nyingi wakaazi wa kaunti hiyo wamekuwa wakijutia baada ya kushirikiana na wanasiasa wadanganyifu na ambao baadaye hutoweka na kushindwa kuimarisha maisha yao mashinani.
Akizungumza katika eneo bunge la Mvita, Nassir amewataka wakaazi kubadili mbinu yao ya kuwachagua viongozi na badala yake washirikine na viongozi waadilifu pekee.
Wakati uo huo amewatahadharisha wakaazi wa kaunti ya Mombasa dhidi ya kugawanyikana na kuchukiana katika misingi ya kisiasa, akiwataka kudumisha amani na uiano.