Picha kwa hisani
Mradi wa nyumba za kisasa za Buxton katika Kaunti ya Mombasa unazidi kukumbwa na utata huku Mbunge wa Mvita Abdulswamad Shariff Nassir akishikilia kwamba mradi huo unatekelezwa kwa maslahi ya mtu binafsi.
Nassir amesema mradi huo utawahangaisha wakaazi wanaoishi katika eneo hilo la Buxton kwa kuwaondoa bila ya kuwatengea maeneo mbadala ya kuishi.
Kulingana na Abdulswamad, Mwanakandarasi anayetekeleza mradi huo anapaswa kukutana moja kwa moja na wakaazi wa nyumba hizo ili kutanzua mgogoro huo.
Mbunge huyo wa Mvita aidha anasema kima cha shilingi laki 2 elfu 40 ambacho wakaazi hao watakabidhiwa ni cha chini na kinastahili kuongezwa.
Hata hivyo, mwekezaji na Mwanasiasa Suleiman Shahbal anayeutekeleza mradi huo wa kima cha shilingi bilioni 6 na unaotarajiwa kuanza mapema mwezi Januari mwakani amewakosoa wanasiasa kwa kuingiza siasa mradi huo.