Story by Gabriel Mwaganjoni –
Mbunge wa Mvita Abdulswamad Sharif Nassir amemtaka Gavana wa Mombasa Ali Hassan Joho kuzuia mgomo wa wahudumu wa afya katika kaunti hiyo kwa kuwalipa mishahara yao.
Nassir amesema Gavana Joho hafai kusalia kimya huku wahudumu wa afya katika kaunti hiyo na wafanyakazi wengine wakifanya kazi bila ya mishahara kwa zaidi ya mwezi tatu.
Akizungumza wakati wa kampeni zake za kuwania ugavana wa Mombasa, Nassir amesema ni kinyume kwa wafanyakazi wa kaunti hiyo kuhangaika ilhali Serikali ya kaunti ina uwezo wa kupigania maslahi yao hadi katika Serikali ya kitaifa.
Wahudumu hao wa afya wakiwemo madaktari, wauguzi, maafisa wa kliniki, na wale wa maabara katika hospitali na zahanati zote za umma wameapa kusambaratisha shughuli za kimatibabu katika kaunti hiyo kuanzia siku ya Jumanne