Picha kwa hisani –
Naibu wa Rais William Ruto ameahidi kushirikiana na Mbunge wa Msambweni Feisal Bader kukamilisha miradi ya maendeleo iliyoidhinishwa na aliyekuwa mbunge wa eneo hilo Marehemu Suleiman Dori.
Akiwahutubia wakaazi wa msambweni hapo jana Ruto amesema ushindi wa Feisal unaashiria mwamko mpya wa uongozi nchini kwani wananchi wanachagua viongozi pasi na kuzingatia mirengo ya kisiasa.
Kwa upande wake Mbunge wa Msambweni Feisal Bader ameahidi kumuunga mkono naibu wa rais William Ruto kwenye azma yake ya kuwania urais wa taifa hili kwenye uchaguzi utakaoandaliwa mwaka 2022.