Picha kwa hisani –
Mbunge wa eneo bunge la Matungu katika Kaunti ya Kakamega Justus Murunga ameaga dunia usiku wa kuamkia leo baada ya kuhisi matatizo ya kupumua.
Marehemu alifikwa na mauti yake wakati alipokuwa akipata matibabu katika hospitali moja kwenye eneo hilo .
Rais Uhuru Kenyatta , Naibu rais William Ruto , Kinara wa ODM Raila Odinga pamoja na Gavana wa kaunti ya Kakamega Wycliffe Oparanya wametuma rambirambi zao kwa familia ya marehemu Murunga.
Aidha ripoti kutoka kwa jamaa wa karibu wa marehemu zimebaini huenda Murunga alifariki kutokana na maambukizi ya virusi vya Corona ambavyo vimepelekea zaidi ya wakenya elfu moja na mia mbili kupoteza maisha .