Mbunge wa Matuga Kassim Sawa Tandaza amewahimiza Viongozi wa Pwani kujitenga na siasa za migawanyika ya vyama na badala yake kuangazia masuala yanayowahusu wananchi moja kwa moja.
Tandaza amesema taifa hili halifai kuendelea kushuhudia siasa za migawanyika ambazo hudidimiza ukanda wa Pwani kuimarika kiuchumi na maendeleo, akisisitiza umuhimu wa viongozi kuja pamoja na kuwahudumia wapwani.
Aidha amedokeza kuwa tabia ya baadhi ya viongozi kuzingatia sana misingi ya vyama hupelekea hata baadhi yao kuhisi kukandamizwa na kukosa kuwatekelezea wananchi masuala muhimu mashinani.
Akigusia suala la Viwanda vya Pwani, Tandaza amewataka viongozi wa Pwani kushirikiana na kupitisha miswada iliyowasilishwa bungeni ya kutaka kufufuliwa upya kwa baadhi ya viwanda eneo hili hasa vinavyohusiana na masuala ya Kilimo.
Taarifa na Hussein Mdune.