Picha kwa hisani –
Mbunge wa Malindi Aisha Jumwa amemkosoa kinara wa ODM Raila Odinga kwa misingi kwamba anatumia mchakato wa kuunganisha wakenya wa BBI kuwahadaa wakenya.
Akihutubia wakaazi katika eneo bunge lake Jumwa amesema kuna haja ya wakenya kupewa muda wa kutosha kuisoma ripoti hio badala ya kuharakishwa kutoa saini pasi na kuelewa kilichomo ndani ya ripoti hio.
Jumwa hata hivyo amepinga vikali kipengele cha nyongeza ya mgao wa fedha kwa kaunti kilichojumuisha kwenye ripoti hio,akisema ugavi huo wa fedha kwa kaunti ungepaswa kutatuliwa bungeni.