Mbunge wa Magarini kaunti ya Kilifi Michael Kingi amehimiza ushirikiano wa viongozi kwa lengo la kuleta maendeleo mashinani.
Kingi amehimiza viongozi kushirikiana kwa karibu ili kuafikia agenda kuu ya maendeleo kwa wakazi wa mashinani.
Aidha amesema suala linalohusu mageuzi ya katiba halifai kutumika kisiasa kuwagawanya viongozi badala yake linafaa kujadiliwa kwa kina ili kuwanufaisha wananchi mashinani.
Mbunge huyo ameahidi kushirikiana vyema na viongozi wa mashinani katika eneo bunge lake ili kuboresha zaidi huduma za maendeleo.
Taarifa na Esther Mwagandi.