Story by Gabriel Mwaganjoni-
Mbunge wa Likoni Mishi Mboko anawataka Maafisa wa polisi katika eneo hilo kukoma kuwahangaisha wahudumu wa Bodaboda.
Mboko anasema wahudumu hao ni vijana wanaojitafutia riziki na tabia ya polisi kuwahangaisha licha ya wahudumu hao kuwa na vibali vyote hitajika kamwe haifai.
Akizungumza katika eneo bunge lake la Likoni, Mboko amesema ni sharti polisi waishi vyema na wahudumu hao ambao wamekuwa mchango mkubwa katika kuwafichua wahalifu katika jamii ya gatuzi hilo dogo la Likoni.