Story by Hussein Mdune –
Mbunge wa Likoni Bi Mishi Mboko ameweka wazi kwamba ukosefu wa sodo kwa mtoto wa kike katika maeneo ya mashinani kumechangia wengi wao kukosa elimu bora.
Akizungumza na Wanahabari baada ya kusambaza sodo kwa wanafunzi wa kike wa shule za upili na msingi katika eneo bunge lake, Bi Mboko amesema idadi kubwa ya wanafunzi wanapitia changamoto nyingi kutokana na ukosefu wa bidhaa hiyo muhimu.
Bi Mboko amesema kwa ushirikiano na wadau mbalimbali wa sekta ya elimuy pamoja na wahisani atahakikisha wanafunzi wa kike wanasalia shuleni kwani itakuwa rahisi kwa bidhaa hiyo kupatikana.
Wakati uo huo amewataka wahisani kujitokeza kushirikiana na jamii mashinani ili kuwasaidia watoto wa kike na bidhaa hiyo muhimu.