Story by Bakari Ali –
Mbunge wa Kisauni Ali Mbogo amewataka viongozi katika kaunti ya Mombasa kuweka mikakati mwafaka ya kutatua mizozo ya ardhi inayowakumba wakaazi wa kaunti hiyo.
Akizungumza katika eneo bunge lake, Mbogo amesema uongozi wa kaunti hiyo unapaswa kuweka mikakati bora ili wakaazi waishi katika ardhi zao bila ya usumbufu.
Mbogo amesema serikali kuu kupitia kamati ya ardhi katika bunge la kitaifa imetenga takriban shilingi milioni 300 kununua kipande cha ardhi cha Junda ili wakaazi hao wagawiwe ardhi hiyo.
Wakati uo huo amewataka wakaazi wa kaunti hiyo kuzingatia kwa kina sheria za umiliki wa ardhi ili kuepuka mizozo ya ardhi inayoshuhudiwa kila mara katika sehemu tofauti za kaunti hiyo.