Story by Gabriel Mwaganjoni –
Mbunge wa Kisauni Ali Mbogo ameweka bayana kwamba amejizatiti katika kulitanzua tatizo sugu la ardhi katika eneo bunge hilo.
Mbogo aliyekuwa akiwahutubia wakaazi wa Kisauni katika kampeni zake za kuwania ugavana wa kaunti ya Mombasa amesema ikilinganishwa na watangulizi wake, amejizatiti kulikabili swala sugu la ardhi na kuwakimu baadhi ya wakaazi kwa hati miliki za ardhi.
Mbogo amesema pindi atakapochanguliwa kama gavana wa kaunti ya Mombasa ataendeleza juhudi za kuzima tatizo la uskwota katika kaunti nzima ya Mombasa.
Mbogo amezidi kuwahimiza wakaazi wa kaunti hiyo kuwa na subra kwani malengo yake ni kuhakikisha kila mkaazi wa kaunti ya Mombasa anaishi katika ardhi yake bila ya hofu yoyote.