Taarifa na Sammy Kamande.
Mbunge wa Kisauni Ali Mbogo amesema uboreshaji wa miundo msingi ikiwemo barabara kutasaidia pakubwa katika kuukabili utovu wa usalama eneo hilo.
Akizungumza wakati wa kukagua ujenzi wa barabara unaoendelea katika wadi ya Shanzu Mbogo amesema ujenzi wa barabara utarahisisha shughuli za usafiri hasa kwa magari ya maafisa wa usalama.
Mbogo vile vile amewataka vijana wa eneo hilo kujitokeza iliwaajiriwe katika mradi huo unaoendelea wa ujenzi wa barabara.