Mbunge wa Kisauni Ali Mbogo ameyalaumu mashirika ya kijamii jijini Mombasa kwa kile alichodai kama kuhusika pakubwa katika kuwapa nguvu vijana kuendeleza msururu wa visa vya kihalifu mitaani.
Mbogo ameeeleza kuwa mashirika hayo hujitokeza pekee wakati mshukiwa wa uhalifu anapouawa lakini huwa kimya, raia wa kawaida wanapoumizwa au kuuawa na majambazi.
Mbogo anasema hali hii imewachochea vijana hasa walio katika makundi ya kihalifu, kuendeleza vitendo vya kihalifu.
Mbunge huyu wa Kisauni ameyahimiza mashirika ya kijamii kushirikiana vyema na idara ya usalama kufanikisha vita dhidi ya uhalifu Kisauni badala ya kukashifu utendakazi wa maafisa hao.
Taarifa na Hussein Mdune.