Story by Charo Banda –
Mbunge wa Kilifi Kaskazini Owen Baya sasa anadai kwamba atawasilisha hoja bungeni ya kuishinikiza serikali ya kitaifa kuondoa kafyu nchini.
Baya anasema kafyu imesambaratisha pakubwa sekta ya Utalii katika ukanda wa Pwani licha ya sekta hiyo kuchangia pato kubwa kwa taifa hili.
Akizungumza kule Malindi, Baya amesema sekta ya Utalii huchangia mapato zaidi nyakati za usiku na kuwepo kwa kafyu nchini kunazidi kudidimiza sekta hiyo ambayo inategemewa na wengi.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa wadau wa sekta ya Utalii kanda ya Pwani Justine Kitsao amepongeza hatua ya serikali ya kaunti ya Kilifi ya kuhakikisha wafanyikazi wote wa hoteli wanapata chanjo ya Corona.