Mbunge wa Kaloleni Paul Katana ameitaka tume ya maadili na kupambana na ufisadi nchini EACC kuidhinisha uchunguzi katika eneo bunge hilo ili kuchunguza fedha zinazodaiwa kupotea katika hazina ya ustawishaji ya eneo bunge hilo.
Katana anaitaka EACC kufanya uchunguzi huo baada ya kudaiwa kuwa mamilioni ya fedha hayajulikani yaliko na huenda zimefujwa.
Katana amewaonya wanakamati wanaosimamia fedha hizo akisema atakayepatikana na hatia atakabiliwa kisheria.
Amewahimiza viongozi kukomesha siasa za malumbano na badala yake washirikiane kuwahudumia wananchi wa Kaloleni.
Taarifa na Mercy Tumaini.