Story by Ephie Harusi –
Mbunge wa Ganze Teddy Mwambire ameitaka serikali ya kitaifa kuweka mikakati dhabiti itakayohakikisha Tume ya kuajiri walimu nchini TSC inawajiri walimu wa kutosha katika eneo bunge hilo ili kuinua viwango vya elimu.
Mwambire amesema idadi kubwa ya walimu katika eneo bunge hilo wamekosa kuajiriwa licha kufadhiliwa na kupata taaluma hiyo kupitia hazina ya CDF.
Akizungumza na Wanahabari, Mwambire amesema hali hiyo imezidi kuongeza mzigo kwa wazazi kwani wanalazimika kuajiri walimu kutokana na upungufu wa walimu wa kutosha shuleni.
Wakati uo huo amesema ukosefu wa walimu wa kutosha umechangia visa vya utovu wa nidhamu kushuhudiwa shuleni, akisema idadi ya walimu inapaswa kuambatana na idadi ya wanafunzi shuleni.