
Mbunge wa Matuga, Kassim Sawa Tandaza. Picha/ Mariam Gao
Mbunge wa Matuga Kassim Sawa Tandaza amewashauri wanandoa kuvumulia wakati kunapotokea changamoto katika familia zao.
Akizungumza na Wanahabari, Tandaza amesema hatua hiyo itasaidia familia nyingi kudhibiti changamoto katika jamii na kuwawezesha kuafikia malengo ya maisha yao ya baadaye.
Amesema kuna masuala mengi ya kisheria ambayo yanahitaji uwepo wa cheti cha ndoa ili kutatua masuala mbalimbali kutoka kwa idara za kiseriakli.
Wakati uo huo amewataka wazazi kuhakikisha wanawashauri watoto wao kuhusu kuzingatia maadili mema ili kutimiza ndoto zao za kielimu.
Taarifa na Mariam Gao.