Taarifa na Gabriel Mwaganjoni
Mombasa, Kenya, Julai 01 – Mbunge wa Changamwe Omar Mwinyi amewakosoa wazazi wa eneo bunge lake kufuatia kudidimia kwa maadili ya watoto katika eneo hilo.
Mwinyi amesema wazazi wa eneo hilo wamejitenga na majukumu ya kuwalea watoto wao kimaadili, hali inayochangia maisha duni ya watoto na vijana wa eneo bunge hilo, akisisitiza haja ya wazazi kuwalea vyema watoto wao.
Kulingana na Mwinyi, bila ya Wazazi kuwajibika na kuwaelekeza watoto wao katika maadili, viwango vya elimu ambavyo tayari viko chini katika eneo hilo vitazidi kusambaratika.