Mbunge wa Magarini kaunti ya Kilifi Michael Thoya Kingi amewashauri wanafunzi kutoka eneo bunge hilo na kaunti yote kwa jumla kuzingatia kikamilifu Elimu.
Akizungumza wakati wa hafla ya kuchangisha pesa kwa wanafunzi wa vyuo vikuu katika wadi ya Marafa eneo bunge la Magarini, Kingi amewataka wazazi kushirikiana vyema na viongozi pamoja na wadau mbali mbali wa sekta ya Elimu ili kufanikisha elimu.
Kingi ameahidi kwamba wanafunzi wote wanaofanya vyema masomoni watapata ufadhili pasi kubaguliwa kwa msingi wowote ili wawezeshwe kutimiza ndoto zao maishani na kuifaa jamii siku zijazo.
Taarifa na Esther Mwagandi.