Rabai, Kenya – Agosti 3 Mbunge wa Rabai William Kamoti ameitaka serikali kuongeza mgao wa hazina ya maendeleo ya maeneo bunge yaani CDF nchini ili hazina hiyo iweze kutosheleza miradi kwa wananchi.
Akiongea kule Rabai wakati wa ufunguzi rasmi wa madarasa mawili katika shule ya Msingi ya Makobeni yaliyofadhiliwa na shirika la Coins for Africa, Kamoti amesema kuwa fedha wanazopewa kwa sasa ni chache mno kutokana na mahitaji ya maeneo bunge nchini.
Mbunge huyo anadai kuwa kutokana na uchache wa fedha hizo wabunge wengi wamekuwa wakitegemea wafadhili ili kuendesha miradi katika maeneo bunge yao.
Kamoti amehoji kuwa kuwa kwa sasa kila eneo bunge hupokea shilingi milioni 100 pekee ambazo ni chache mno ikilinganishwa na majukumu ya maeneo bunge nchini.