Wahudumu wa Bodaboda katika eneo la Kaloleni kaunti ya Kilifi, wameandamana kupinga unyanyasaji na kuhangaishwa na maafisa wa polisi eneo hilo.
Wakiongozwa na Kiongozi wao Festus Kazungu, wahudumu hao wa bodaboda wamesema afisa anayesimamia kituo cha polisi cha Kaloleni amekuwa akiwaongoza maafisa wenzake kuwahangaisha bodaboda hao kila uchao.
Akizungumza na Vijana hao nje ya ofisi za CDF kule Kaloleni, Mbunge wa Kaloleni Paul Katana ametoa makataa ya siku 14 kwa Afisa huyo anayesimamia kituo hicho kupewa uhamisho.
Akijubu shtuma hizo, Afisa mkuu wa Polisi eneo hilo Kennedy Osando amesema swala hilo litashuhulikiwa huku akiwashauri vijana hao kuwa na uvumilivu kwani usalama wao pia unazingatiwa.
Taarifa na Mercy Tumaini.