Taarifa na Mercy Tumaini
Mbunge wa Kaloleni Paul Katana amesema kuna haja ya maafisa wa usalama kupewa ushauri wa kisaikolojia wakati wanapomaliza mafunzo.
Katana amesema kuanzishwa kwa mpango huo katika vituo vya mafunzo ya usalama kutakabiliana na visa vinavyoshuhudiwa vya maafisa wa polisi kujipiga risasi ama kujiua.
Akizungumza na wanahabari kule Kaloleni, Katana amesema visa hivyo vinazidi kushuhudiwa nchini, kisa cha hivi majuzi ikiwa ni afisa wa polisi wa kituo cha polisi cha Kizurini kupijiga risasi na kufariki.
Hata hivyo polisi wamedai kuanzisha uchunguzi kuhusiana na tukio hilo huku Mwili wa mwendazake unahifadhiwa katika hifadhi ya maiti ya hospitali kuu ya ukanda wa Pwani.