Taarifa na Sammy Kamande.
Mbunge wa kisauni Ali mbogo ameitaka serikali kumteua mwenyekiti wa tume ya kitaifa ya ardhi mara moja ili kuwawezesha viongozi kutatua mizozo ya ardhi inayoshuhudiwa katika maeneo mbali mbali ya nchini.
Kulingana na Mbogo ukosefu wa mwenyekiti wa tume hio umechangia changamoto zinazoshuhudiwa katika kutatua migogoro ya ardhi inayokumba wananchi.
Ameshikilia kwamba iwapo kutateuliwa mtu muafaka wa kushikilia wadhfa huo mizozo ya ardhi itakomeshwa.