Taarifa na Alphalet Mwadime
Mombasa, Kenya, Juni 26 – Mbunge wa Mvita Abdulswamad Shariff Nassir amesema takwimu zilizotolewa hivi majuzi na mamlaka ya kukabiliana na mihadarati na vileo haramu nchini NACADA ni za kutisha.
Abdulswamad amesema takwimu hizo zinazobainisha kwamba asilimia 16.9 ya watoto wa shule ya msingi wamejitosa katika uraibu wa dawa za kulevya inatia wasiwasi na ni sharti hatua za haraka zichukuliwe ili kuidhibiti hali hiyo.
Kulingana na Abdhulswamad ni lazima Serikali ijizatiti katika kuudhibiti ulanguzi wa dawa za kulevya humu nchini sawia na kutumia sheria zilizopo katika kuidhibiti hali hiyo tata.
Amesema japo kumekuwepo na haratakati za kukabiliana na utumizi wa dawa za kulevya miongoni mwa Wakaazi wa Ukanda wa Pwani, juhudi hizo hazijaungwa mkono ipasavyo na serikali.