Story by Gabriel Mwaganjoni –
Wagombea wawili wa ugavana wa kaunti ya Mombasa ambao ni Mbunge wa Kisauni Ali Mbogo na Naibu Gavana wa Mombasa Dakta William Kingi wameashiria kuungana kisiasa katika kuwabwaga wapinzani wao wa karibu Mfanyabiashara Suleiman Shahbal na Mbunge wa Mvita Abdulswamad Sharif Nassir.
Katika mazungumzo ambayo bado hayajawekwa wazi, Mbogo ameonekana kushirikiana kwa karibu na Kingi katika mikutano yake ya kisiasa na hata kufanya mikutano kadhaa ya kisiasa wakiwa Pamoja.
Wakizungumza katika mikutano yao ya kisiasa katika Gatuzi dogo la Kisauni, Kingi na Mbogo wamewataka wakaazi wa kaunti hiyo kutofanya makosa ya kuwachagua viongozi wasio kuwa na nia ya kuinua maisha yao.
Wakazi uo huo, Kingi amepuuzilia mbali uongozi wa Nassir akisema hajatekeleza mradi wa maana katika kipindi cha miaka 10 ambacho amehudumu kama Mbunge wa Mvita.