Taarifa na Sammy Kamande.
Mbunge wa kisauni Ali Mbogo amesema utumizi wa dawa za kulevya miongoni mwa vijana wa kaunti hiyo utakomeshwa iwapo vitengo mbali mbali vya serikali vitashirikiana.
Kulingana na Mbogo miradi mbali mbali inayowalenga vijana inayoidhinishwa na serikali imesaidia pakubwa katika kumaliza tatizo la mihadarati kaunti hiyo.
Ameitaka serikali kuu na ile ya kaunti ya Mombasa kushirikiana na mabalozi wa nyumba kumi na kuhakikisha walanguzi wa dawa za kulevya wanafichuliwa.