Story by Bakari Ali –
Mbunge wa Kisauni Ali Mbogo ameitaka Serikali ya kaunti ya Mombasa kuwajibika ipasavyo katika kuliangazia swala uzoaji wa taka katika kaunti hiyo.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa barabara ya Mombasa -Mwakirunge, Mbogo amesema serikali ya kaunti ya Mombasa imezembea katika swala la kudhibiti mirundiko ya taka.
Mbunge huyo wa Kisauni amesema hali hiyo imechangia kushuhudiwa maeneo mbalimbali ya kaunti hiyo mirundiko ya taka hali ambayo huenda ikachangia madhara kwa binadamu.
Mbogo amesema amewekeza ipasavyo kupitia hazina ya ustawi wa eneo bunge hilo CDF katika kuboresha hali za barabara zinazotumika kusafirisha taka katika eneo bunge hilo.