Story by Gabriel Mwaganjoni –
Mbunge wa Kisauni Ali Mbogo amemshambulia Gavana wa Mombasa Ali Hassan Joho na kusema kwamba hafai kuongoza kaunti ya Mombasa kwani amekosa malengo ya maendeleo.
Mbogo aliyekuwa akiwahutubia wakaazi katika eneo la Shanzu, amesema ni aibu kwa Wafanyakazi wa kaunti hiyo kufanya kazi hadi miezi mitatu bila ya mishahara hali inayowafanya watu hao kuishi maisha ya taabu.
Mbogo amemtaka Joho kutambua majukumu yake kama Kiongozi wa kaunti hiyo na kujali maslahi ya wafanyakazi na wala sio kujihusisha na maswala yasiokuwa na umuhimu wowote kwa kaunti hiyo.
Mbunge huyo wa Kisauni ameapa kutorudi nyuma katika azma yake ya kuwania ugavana wa kaunti ya Mombasa katika uchaguzi mkuu wa Agosti 9, mwaka huu.