Story by Gabriel Mwaganjoni
Uongozi wake Mgombea wa ugavana wa kaunti ya Mombasa Mike Mbuvi Sonko na mgombea mwenza wake Ali Mbogo utaleta mabadiliko msingi ya maendeleo kwa wakaazi wa kaunti hiyo.
Haya ni kulingana na Mbogo ambaye pia ni Mbunge wa Kisauni, aliyesmea ni sharti kaunti ya Mombasa ipate uongozi bora na utakaomjali kila mkaazi na wala sio uongozi wa kuwapendelea watu fulani na kuwabagua wengine.
Wakizungumza katika eneo la Shanzu katika kaunti ya Mombasa, Mbogo amesema hawatarudi nyuma katika azma yao ya kuikomboa kaunti ya Mombasa.
Wakati uo huo amewarai wakaazi wa Mombasa kutoingiwa na hofu yoyote wala kutotishiwa na mirengo fulani ya kisiasa na badala yake kuunga mkono juhudi zake na Sonko katika kuufanikisha mchakato wa kimaendeleo katika kaunti hiyo.