Mazishi ya mchezaji soka nguli Joe Kadenge yatagharimu kima cha shillingi milioni tano pesa za Kenya hii ni sawa na dola za marekani elfu 50.
Kulingana na familia ya mwendazake mazisHi yatafanyika tarehe 20 mwezi huu wa Julai nyumbani kwake Hamisi, Kaunti ya Vihiga.
Mwili wa marehemu utasafirishwa kwa ndege siku ya Alhamisi hadi Kisumu kabla ya kusafiri kwa gari hadi nyumbani kwake.
Jumatano ya tarehe 17 mwezi huu wa Julai kutakuwa na ibada ya wafu katika kanisa la Friends International Jijini Nairobi.