Waziri wa Utalii nchini Najib Balala ameeleza haja ya kuboreshwa kwa mazingira ya viwanja vya ndege nchini ili kuinua viwango vya Utalii.
Akihutubu kwenye Kongamano lililowaleta pamoja wadau wa Shirika linalohusika na uchukuzi wa angani kutoka mataifa ya Bara la Afrika, Waziri Balala amesema viwanja vingi vya ndege barani Afrika havina mazingira bora ya kuwapokea watalii.
Amesema kuna haja ya mataifa hayo kuekeza na kuidhinisha sheria mwafaka zitakazotoa vikwazo kwa wageni wanaozuru mataifa ya Afrika kutalii ili kuimarisha zaidi sekta hiyo.
Kwa upande wake Mkurugenzi mkuu wa Mamlaka ya kitaifa kuhusu urubani nchini Gilbert Kibe amedokeza kuwa Shirika hilo litajadili kwa kina swala hilo ili kuhakikisha shughuli za uchukuzi wa angani zinaboreshwa zaidi.
Taarifa na Cyrus Ngonyo.
Taarifa n Cyrus Ngonyo.